Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

BIASHARA YA USAFIRISHAJI MAJINI

Imewekwa: 02 February, 2023
BIASHARA YA USAFIRISHAJI MAJINI

Biashara ya Huduma za Meli

KURUGENZI YA BIASHARA HUDUMA ZA MELI

Kurugenzi ya Biashara huduma za meli inatekeleza majukumu ya Uwakala wa forodha chini ya sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania kifungu namba 7 Sura 415.

1.0 UWAKALA WA FORODHA

TASAC ilianza kutekeleza majukumu ya Uwakala wa Forodha mnamo tarehe 3 Juni, 2019.

TASAC kupitia kitengo cha Uwakala wa Forodha imepewa mamlaka ya kipekee kugomboa na kuondosha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu 7(1) Sura 415.

1.1 Bidhaa za kipekee zinazogombolewa na TASAC ni

  • Makinikia,
  • Silaha,
  • Nyara za Serikali na Wanyama Hai kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori,
  • Kemikali zinatumiwa na makampuni ya uchimbaji madini

1.2 KAZI ZA KITENGO CHA UWAKALA WA FORODHA

  • Kupokea na kukagua nyaraka kutoka kwa waagizaji na wauzaji mizigo
  • kuandaa Kadhia na kuzituma kwenye mifumo ya forodha kwa makadirio ya kodi
  • Kuwasiliana na mteja kwa ajili ya maombi na ufuatiliaji wa vibali kutoka mamlaka nyingine za Serikali
  • Kuomba ankara za malipo na kufuatilia nyaraka kutoka kwa Wakala wa Meli
  • Kushiriki kwenye ukaguzi wa shehena katika maeneo ya kiforodha na masoko ya madini
  • Kuwasiliana na bandari kwa maombi ya Ankara za malipo
  • Kuwashauri na kuwaelimisha wateja kuhusu taratibu za kiforodha
  • Kuratibu uondoshwaji wa shehena kwakuzingatia taratibu za mamlaka zakiudhibiti

1.3 MAENEO YA UWAKALA WA FORODHA

Huduma za uwakala wa forodha zinafanyika katika maeneo yafuatayo:

  • Bandari
  • Viwanja vya ndege
  • Mipakani na,
  • Maeneo mengine kama itakavyo idhinishwa na mamlaka ya forodha

1.4 MAWASILIANO

Jinsi ya kuwasiliana na TASAC kwa huduma za uwakala wa forodha,

Baruapepe

1. Huduma kwa waagizaji wa bidhaa importcfa@tasac.go.tz

2. Huduma kwa bidhaa ziendazo nje ya nchi exportcfa@tasac.go.tz.

3. Huduma za vibali group.cfatbs@tasac.go.tz

4. Huduma kwa mawakala wa meli group.cfashipping@tasac.go.tz

Namba ya simu +255737 792 444

Mrejesho, Malalamiko au Wazo