Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Majukumu na Kazi

Majukumu na kazi

Majukumu na kazi

Kazi na Wajibu wa TASAC vimeelezwa kwenye Sheria ya Shirika.

WAJIBU:

(a) Kuhimiza usimamizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi;

(b) Kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi;

(c) Kuhakikisha Usalama na Ulinzi wa shehena;

(d) Kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito;

(e) Kuhimiza ufanisi, uchumi na uaminifu;

(f) Kuendeleza upanuzi wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji;

(g) Kuhimiza ushindani katika biashara ya uwakala wa meli; na

(h) Kuingia kwenye majukumu ya kimkataba na watu wengine au kikundi cha watu.

KAZI:

Kwa mujibu wa kifungu cha 11- 12 cha Sheria ya TASAC Na. 14 ya mwaka 2017, kazi za Shirika ni:

(1) Kudhibiti Usimamizi wa Shughuli zUsafiri kwa Njia ya Maji, Mazingira, Usalama na Ulinzi

(a) Kusimamia Sheria ya meli za Biashara;

(b) Kutimiza wajibu wa kukagua meli zote za kigeni katika bandari zetu na meli zilizosajiliwa Tanzania Bara;

(c) Kusimamia na kuidhinisha vifaa vya huduma za usalama na watoa huduma za usafiri kwa njia ya maji;

(d) Kusimamia vivuko

e) Kuratibu shughuli za utafutaji na uokozi kwenye bahari, maziwa na mito;

(f) Kusimamia na kuratibu ulinzi na uhifadhi wa mazingira ya bahari, maziwa na mito;

(g) Kutoa taarifa na kujenga uelewa kuhusu mambo yanayohusu mazingira, usalama na ulinzi wa usafiri kwa njia ya maji; na

(h) Kufanya kazi nyingine kama zilivyokasimiwa Shirika kwa mujibu wa Sheria.

(2) Kudhibiti Huduma za Usafirishaji Majini

(a) Kutoa, kuongeza muda na kufuta leseni;

(b) Kuweka viwango vya kudhibiti bidhaa na huduma za kisheria;

(c) Kuweka vigezo na masharti kwa huduma na bidhaa zinazodhibitiwa;

(d) Kudhibiti viwango vya tozo;

(e) Kufuatilia utendaji wa watoa huduma wanaotambulika kisheria;

(f) Kuwezesha ufumbuzi wa malalamiko na migogoro;

(g) Kufuatilia na kusimamia mwenendo wa kampuni za meli na

watoa huduma wengine wanaotambulika kisheria;

(h) Kufuatilia viwango tozo na malipo ya ziada kwa wanaokiuka ili

uhakikishaji matumizi sahihi katika kipindi cha uhalali wa kutumika;

(i) Kuhimiza, kusajili na kutathmini viwango vya tozo za shehena, sarafu na maghala na gharama nyingine au kutoza wanaokiuka kuhusiana na huduma za usafirishaji majini;

(j) Kuzitaka meli zote zinazopakia na kupakua shehena kwenye bandari za Tanzania Barua kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa.

ZINGATIA: Pamoja na kazi zilizoainishwa, TASAC inaweza kufanya kazi nyingine kama Waziri mwenye dhamana atakavyoipangia.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo