Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Misingi Mikuu

MISINGI MIKUU:

(i) Uwajibikaji:

Kuwajibika kwa Taifa letu na kwa wadau katika kutekeleza mamlaka na makujumu yaliyo chini ya dhamana ya Shirika;

ii) Uadilifu:

Kuwa mfano wa kuigwa katika mwenendo wetu wa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwenye shughuli zetu zote;

iii) Utaalamu:

Kutumia mkabala unaodhihirisha utaalamu katika weledi, mwenendo, mtazamo na tabia

iv) Haki:

Kutokuwa na upendeleo katika kutekeleza shughuli zetu kwa wateja, watoa huduma na wadau wengine kwa kutoa huduma bila ya upendeleo wala ubaguzi;

v) Uwazi:

Kuwa wazi katika shughuli zetu zote na kuwa tayari kupokea maoni ya wananchi;

vi) Ubunifu:

Tunajitahidi daima kufikia na kutumia teknolojia na njia mpya za ubunifu wa utekelezaji wa mamlaka na dhamana tuliopewa katika kuchangia maendeleo ya Taifa letu.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo