Udhibiti wa Usafiri kwa Njia ya Maji
Udhibiti wa Usafiri kwa Njia ya Maji
TASAC imejidhatiti kuhakikisha huduma za usafirishaji kwa njia ya maji zinatolewa kwa ubora, ufanisi na kwa wakati. Huduma za udhibiti zimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni udhibiti huduma za bandari na udhibiti huduma za usafirishaji kwa njia ya meli.
Katika Sehemu ya Udhibiti Huduma za Bandari, watoa huduma wanaohudumiwa ni;
- Waendeshaji wa Bandari (Port and Terminal Operators);
- Bandari Kavu (Dry ports);
- Watoa Huduma ndogo ndogo za bandari (Miscellaneous Port Services (MPS providers));
- Wahakiki wa Uzito wa Mizigo ya Makasha (Gross Mass Verifiers (GMV)).
Katika Sehemu ya Udhibiti Huduma za Usafirishaji kwa njia ya meli, watoa huduma wanaohudumiwa ni;
- Mawakala wa Meli (Shipping Agents);
- Wakusanyaji na watawanyaji wa Mizigo (Consolidators/ De-Consolidators);
- Wakala wa Ugomboaji na Uondoshwaji wa Mizigo (Clearing and Forwarding Agents).
Katika sehemu zote zilizotajwa hapo hapo juu, TASAC hutoa huduma za udhibiti na kuhakikisha uzingatiaji wa yafuatayo;
- Utoaji, uhuishaji na ufutaji wa leseni;
- Uwekaji viwango vya bidhaa zinazodhibitiwa na huduma zinazodhibitiwa;
- Uwekaji vigezo na masharti ya kutoa bidhaa na huduma zinazodhibitiwa;
- Udhibiti tozo na malipo;
- Ufuatiliaji wa utendaji wa watoa huduma wanaodhibitiwa;
- Uwezeshaji wa utatuzi wa malalamiko na migogoro;
- Ufuatiliaji na usimamiaji wa tabia na mienendo ya wenye meli na watoa huduma wengine wanaodhibitiwa;
- Usimamiaji wa nauli za mizigo na malipo mengine ili kuhakikisha kuna matumizi sahihi wakati wa kipindi cha uhalali wake;
- Uitishaji, uorodheshaji na tathmini ya nauli za mizigo, gharama za ziada zinazohusu mabadiliko ya thamani ya sarafu na mabadiliko ya bei za mafuta na tozo zingine au tozo za ziada zinazohusiana na usafiri kwa njia ya maji;
- Kuzitaka meli zote zinazopakia na kupakua mizigo kwenye bandari za Tanzania Bara kuwasilisha kwa TASAC taarifa zifuatazo;
-
- Taarifa za Meli,
- Nauli za mizigo,
- Nakala za 'manifest' zinazoonyesha nauli za mizigo na mikataba ya ukodishaji meli kwa mizigo inayoingizwa na kutoka nje ya nchi,
- Nakala za makubaliano ya utendaji au huduma,
- Taarifa ya kuwekwa kwa malipo yoyote mapya,
- Masharti ya huduma na,
- Taarifa nyingine yoyote inayohusiana.
- Kusajili wasafirishaji, mawakala wa meli na mawakala wa ugomboaji na uondoshwaji wa mizigo;
- Kusimamia mwenendo wa mawakala wa meli;
- Kusambaza taarifa kuhusu masuala yanayohusiana na majukumu ya TASAC; na
- Kufanya majukumu yoyote kama yanavyoweza kusimamiwa na Shirika kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania na Sheria zingine.
Huduma za kiudhibiti zilizotajwa hapo juu pia zinapatikana kwa njia ya mtandao Shipping Service Providers Online Portal, makao makuu na ofisi za mikoa.