TASAC YAWAHIMIZA WATOA HUDUMA USAFIRI MAJINI KUZINGATIA USALAMA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa wito kwa watoa huduma ya usafiri majini wanaojishughulisha na kubeba abiria kati ya Dar es Salaam na Zanzibar kuzingatia masharti ya leseni za vyombo waliyopewa.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Usalama, Ulinzi wa Vyombo vya Usafiri Majini na Utunzaji wa Mazingira, Mhandisi Lameck Sondo, leo tarehe 12 Agosti, 2025, wakati wa ukaguzi wa boti zinazotoa huduma ya usafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.
Mha. Lameck Sondo amesema kuwa TASAC hufanya shughuli za ukaguzi wa vyombo ili kuona kama vinatimiza masharti ya leseni zao na kutaja kuwa kaguzi za kushtukiza zinafanywa kwa lengo la watoa huduma kuzingatia kanuni na taratibu za usalama wa usafiri majini.
"Leo, tumefanya ukaguzi kuona kama abiria waliokatiwa tiketi na kusafirishwa ni sawa na uwezo wa vyombo vya usafiri majini, kwani tunafahamu muda wa asubuhi uwa na wasafiri wengi, hivyo, mahitaji ya usafiri huongezeka sana," amesema Mha. Sondo.
Ameongeza kuwa ni takwa la kisheria kwa watoa huduma wote wa usafiri majini nchini kutoa huduma kwa kufuata masharti ya leseni, kanuni na sheria za usalama wa usafiri majini na matumizi ya vifaa okozi.
kwa watoa huduma wote wa usafiri majini nchini kutoa huduma kwa kufuata masharti ya leseni, kanuni na sheria za usalama wa usafiri majini na matumizi ya vifaa okozi.
Zoezi la ukaguzi wa usalama wa usafiri majini ni endelevu kwa nchi nzima na hufanya kwa namna tofauti ikiwemo hii ya kushtukiza. Tunaomba abiria kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano mara wanapowaona maafisa wa TASAC wakiingia kwenye vyombo hivyo.
Zoezi la ukaguzi wa usalama wa usafiri majini ni endelevu kwa nchi nzima na hufanywa kwa namna tofauti ikiwemo hii ya kushtukiza.
TASAC inatoa wito kwa abiria kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano mara wanapowaona maafisa wa Shirika wakifanya kaguzi kwenye vyombo vya usafiri majini nchi nzima.
Ameongeza kuwa ni takwa la kisheria