Biashara ya Huduma za Meli

KURUGENZI YA BIASHARA HUDUMA ZA MELI

Kurugenzi ya Biashara huduma za meli inatekeleza majukumu yake chini ya sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania kifungu namba 7 Sura 415.
Kurugenzi imegawanyika katika sehemu kuu tatu:
1.Uwakala wa forodha
2.Uwakala wa meli
3.Uhakiki wa shehena

1.0 UWAKALA WA FORODHA

TASAC ilianza kutekeleza majukumu ya Uwakala wa Forodha mnamo tarehe 3 Juni, 2019.

TASAC kupitia kitengo cha Uwakala wa Forodha imepewa mamlaka ya kipekee kugomboa na kuondosha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu 7(1) Sura 415.

1.1 Bidhaa za kipekee zinazogombolewa na TASAC ni

 • Madini,
 • Makinikia,
 • Mashine na Vifaa kwa ajili ya uchimbaji wa madini,
 • Bidhaa zinazotokana na mafuta ghafi ya petroli,
 • Silaha na Vilipuzi,
 • Wanyama Hai,
 • Nyara za Serikali
 • Mbolea,
 • Sukari ya Viwandani na Nyumbani,
 • Mafuta ya Kula,
 • Ngano,
 • Bidhaa za Mafuta na Vilainishi,
 • Gesi
 • Kemikali
 • Bidhaa nyingine yoyote kama itakavyoamriwa na Waziri mwenye dhamana kwa kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali

1.2 KAZI ZA KITENGO CHA UWAKALA WA FORODHA

 • Kupokea na kukagua nyaraka kutoka kwa waagizaji na wauzaji mizigo
 • kuandaa Kadhia na kuzituma kwenye mifumo ya forodha kwa makadirio ya kodi
 • Kuwasiliana na mteja kwa ajili ya maombi na ufuatiliaji wa vibali kutoka mamlaka nyingine za Serikali
 • Kuomba ankara za malipo na kufuatilia nyaraka kutoka kwa Wakala wa Meli
 • Kushiriki kwenye ukaguzi wa shehena katika maeneo ya kiforodha na masoko ya madini
 • Kuwasiliana na bandari kwa maombi ya Ankara za malipo
 • Kuwashauri na kuwaelimisha wateja kuhusu taratibu za kiforodha
 • Kuratibu uondoshwaji wa shehena kwakuzingatia taratibu za mamlaka zakiudhibiti

1.3 MAENEO YA UWAKALA WA FORODHA

Huduma za uwakala wa forodha zinafanyika katika maeneo yafuatayo:

 • Bandari
 • Viwanja vya ndege
 • Mipakani
 • Masoko ya madini na
 • Maeneo mengine kama itakavyo idhinishwa na mamlaka ya forodha

1.4 MAWASILIANO

Jinsi ya kuwasiliana na TASAC kwa huduma za uwakala wa forodha,

Baruapepe

1. Huduma kwa waagizaji wa bidhaa importcfa@tasac.go.tz

2. Huduma kwa bidhaa ziendazo nje ya nchi exportcfa@tasac.go.tz.

3. Huduma za vibali group.cfatbs@tasac.go.tz

4. Huduma kwa mawakala wa meli group.cfashipping@tasac.go.tz

Namba ya simu +255737 792 444

2.0. UWAKALA WA MELI

TASAC ilianza kutekeleza majukumu ya Uwakala wa meli mnamo tarehe 3/2/ 2020. Majukumu ya kipekee ya uwakala wa meli yamegawanyika katika makundi makuu matatu ikiwemo aina za meli, aina ya shehena iliyobebwa na meli pamoja na masharti ya uendeshaji wa biashara ya meli.

(a) Kwa kuzingatia aina za meli

i). Meli za mafuta

ii). Meli za kukodi

iii). Meli za magari

iv). Meli za Kitalii

v). Meli za maonyesho

vi). Meli zinazoingia nchini kwa mahitaji maalum

vi). Meli za kijeshi

(b) Kwa kuzingatia aina ya shehena iliyobebwa na meli

i). Madini;

ii). Makinikia;

iii). Mashine na Vifaa kwa ajili ya uchimbaji wa madini,

iv). petroli;

v). Silaha na vifaa vya kivita;

vi). Wanyama hai;

vii). Nyara za Serikali;

viii). Mbolea;

ix). Sukari ya viwandani na majumbani;

x). Mafuta ya kupikia;

xi). Ngano;

xii). Bidhaa za mafuta;

xiii). Gesi;

xiv). Gesi ghafi;

xv). kemikali

xvi). Bidhaa nyingine yoyote kama itakavyoamriwa na Waziri mwenye dhamana kwa kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali

(c) Kwa kuzingatia masharti ya uendeshaji wa biashara ya meli

TASAC pia imepewa majukumu ya uwakala wa meli kwa baadhi ya meli zinazoshusha au kupakia mzigo katika bandari za Tanzania bara kwakuzingatia masharti ya uwendeshaji mfano meli za kukodi.

2.1 MAJUKUMU YA TASAC KAMA WAKALA WA MELI

Kifungu Na.6 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania Sura 415 kinaelezea majukumu ya wakala wa meli kwenye kutekeleza shughuli za uwakala wa meli kama ifuatavyo.

a. Kumwakilisha mwenye meli katika biashara ya meli;

b. Kuratibu ujio na kuondoka kwa meli;

c. Kuratibu upatikanaji wa huduma mbalimbali anazohitaji mwenye meli kutoka kwa watoa huduma za bandari, forodha, taasisi nyingine za Serikali na makampuniau watu binafsi;

d. Kuratibu shughuli za usambazaji wa nyaraka za mizigo kwa wateja na wadau wa bandari kama vile “bill of lading” na “delivery order” na pia kuingiza kwenye mfumo wa forodha nyaraka ya orodha ya mizigo iliyobebwa melini (manifest); orodha ya upakiaji au upakuaji mizigo na mpangilio wa mizigo melini (stowage plan);

e. Kuratibu shughuli za usambazaji wa nyaraka za meli zinazohusu kuingia na kutoka kwa melibandarini;

f. Kuratibu na kuandaa nyaraka za mizigo inayotoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kutengeneza “bill of lading”;

g. Kufanya shughuli zote zinazohusu uondoshaji wa meli bandarini;

h. Kuratibu upatikanaji wa huduma zote zinazohusu ubadilishaji wa wafanyakazi wa meli (crew change);

i. Kuratibu upatikanaji wa huduma mbalimbali zinazohitajika melini kama vile vyakula, maji, matengenezo ya meli na huduma nyinginezo;

j. Kuratibu shughuli ya usafirishaji wa shehena zinazoendelea na safari ikiwemo shehena iliyozidi au kupungua kiwango kilichotajwa kwenye nyaraka za mizigo;

k. Kuratibu shughuli ya upakiaji na upakuaji wa shehena kwenye makasha;

l. Kukodi ghala au stookwa ajili ya kuhifadhia mizigo inayosubiri kusafirishwa;

m. Kutafuta masoko na mizigo ya kusafirisha kwenda nje ya nchi nakutangaza huduma zetu za uwakala wa meli kwa niaba ya wenye meli, watoa huduma na wakodishaji;

n. Kutoa taarifa kwa mwenye meli kuhusu maombi ya nafasi ya kupakia mzigo kwenye meli; matumizi ya nafasi iliyoombwa kwa ajili ya kupakia mizigo melini na takwimu kuhusu upatikanaji wa mizigo;

o. Kushughulikia malalamiko kwa niaba ya wenye meli;

p. Kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wenye melikuhusu utendaji wa meli zao pindi zinapokuwa bandarini;

q. Kusimamia, kufuatilia na kuratibu shughuli zote zinazohusu usafirishaji wa makasha tupu na yenye mzigo;

r. Kutunza vizuri kumbukumbu zote zinazohusu miamala ya kifedha inayohusu biashara za meli inayofanywa na wenye meli yakiwemo malipo ya tozo za bandari;

s. Kufanya malipo ya huduma na bidhaa mbalimbali zinazohitajika melini kwa niaba ya wenye meli;

t. Udhibiti wa nyaraka za meli na mizigo yote inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari

2.2 MAENEO YA SHUGHULI ZA UWAKALA WA MELI

Hudumau za uwakala wa meli zinafanyika katika maeneo ya bandari husika

Mawasiliano

Jinsi ya kuwasiliana na TASAC kwa huduma za uwakala wa meli,

Baruapepe: shippingagency@tasac.go.tz


1.0 UHAKIKI WA SHEHENA

Kitengo cha uhakiki wa shehena kilianziashwa kwa lengo kuu la kuhakiki mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari za Tanzania bara.

Majukumu ya kipekee ya uhakiki wa shehena yanatekelezwa chini ya kifungu cha sheria namba 7(1)C cha Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Sura 415.

Kazi ya uhakiki wa shehena ilianza rasmi tarehe 17/02/2020.

3.1 KAZI ZA UHAKIKI WA SHEHENA

Uhakiki wa shehena unahusisha:

 • Kupokea nyaraka za awali zinazohusiana na uhakiki wa shehena husika
 • Uhakiki wa shehena
 • Ulinganishwaji wa taarifa za awali na zile za uhakiki
 • Kuandaa taarifa mbalimbali za uhakiki ikiwa ni pamoja na
 • Taarifa ya “shift”
 • Taarifa ya siku
 • Taarifa ya utendaji wa meli
 • Taarifa za matukio yatokanayo na utekelezaji

Mawasiliano: Barua pepe:shiptallying@tasac.go.tz