Udhibiti wa Usafirishaji Majini

Idara hii inatoa huduma zifuatazo;

 1. Kutengeneza kanuni na viwango vya udhibiti wa huduma za bandari na usafirishaji majini;
 2. Kuhamasisha huduma za bandari na usafirishaji majini;
 3. Kuhamasisha usafirishaji unaofaa na nchi zisizo na bandari;
 4. Kutoa leseni za Mawakala wa huduma za usafirishaji majini;
 5. Kuhakikisha watoa huduma wanatoza viwango kwa mujibu wa kanuni zilizopo;
 6. Kufanya vikao vya ushauriano na wadau wa sekta hii;
 7. Kuhimiza kukidhi kwa tabia na mwenendo bora kwa watoa huduma za bandari na usafirishaji majini;
 8. Kuhamasisha matumizi bora ya usafirishaji majini katika Maziwa makuu na usafirishaji unaofaa;
 9. Kuimaimarisha usafirishaji wa ndani wa bara wenye ushindani; na
 10. Kudhibiti huduma za mawakala wa usafirishaji majini, kampuni za meli, shughuli za bandari, mawakala wa upokeaji, usafirishaji na wakusanyaji shehena.

USAJILI

Usajili wa Mawakala wa Upokeaji na Usafirishaji Shehena

Mawakala wote wa Upokeaji na Usafirishaji Shehena wanatakiwa wajisajili TASAC kwa mujibu wa Sheria ya TASAC Na. 14 ya 2017. Fomu zinajazwa nakala mbili. Bofya kupata fomu ya Usajili.

USAJILI WA UKASANYAJI WA SHEHENA

Kanuni na masharti ya usajili

Mwombaji lazima awe na:-

 1. Ofisi isiyopungua ukubwa wa mita za mraba 18;
 2. Kampuni iliyosajiliwa yenye hisa nyingi za watanzania;
 3. Eneo la kukusanyia shehena;
 4. Vifaa vya mawasiliano, hasa simu ya mezani, nukushi, barua pepe, n.k;
 5. Uwezo na ujuzi wa kushughulikia bidhaa zinazoingiwa na zinasafirishwa nchi za nje;
 6. Watumishi wenye ujuzi kwenye usafirishaji wa shehena;
 7. Viwango vya tozo.