Ziara ya Mafunzo.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge akipokea bango la ukumbusho kutoka kwa Naibu Ufuatiliaji Meli za Biashara kutoka Walinzi wa Pwani ya Marekani (U.S. Coast Guard), Bi. Julieth Hudson ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani katika kuimarisha usalama wa Sekta ya Usafiri kwa Njia ya Maji.
Bw. Mkeyenge amepokea bango hilo wakati wa ziara ya mafunzo nchini Marekani kuanzia tarehe 30 Januari hadi 3 Februari 2023. Katika ziara hiyo ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bahari Zanzibar (ZMA) na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC).
Ziara hiyo ya mafunzo ina lengo la kubadilishana uzoefu wa njia bora za usalama wa bandari.