Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yashiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Imewekwa: 22 March, 2023
TASAC yashiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wameungana na Wanawake wote Duniani katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam tarehe 08/3/2023.  Kauli Mbiu ya mwaka huu ni *UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJI, Chachu katika kuleta usawa wa jinsia. 

Mgeni Rasmi  katika maadhimisho hayo, Mhe. Amosi Makala Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alielezea matumizi ya teknolojia yalivyosaidia mesaidia kuleta usawa katika kufanya kazkatika Karne hiii ambapo kwa sasa wanawake wanaweza kufanya kazi zote bila kubagua.

Aidha,  aliongeza kuwa Tanzania inaungana na Dunia nzima kusheherekea siku hii sababu Maadhimisho haya yanajenga hamasa na ushiriki katika kuchangia na kuleta usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wanawake kwa kuongeza msukumo wa ushiriki wao katika uongozi.

Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi kwa wote walioshiriki Maadhimisho na kutoa rai ya kudumisha umoja katika kutekeleza majukumu yao ili kukuza uchumi wa Taifa.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo