WIZARA YA UCHUKUZI YAFANYA KIKA NA WADAU CHA KUPOKEA MAONI KUHUSU MWONGOZO WA UCHANGIAJI HUDUMA ZA AFTA MIPAKANI

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASC) imeratibu kikao cha wadau mbalimbali Sekta ya Uchukuzi ili kupokea maoni kuhusu mwongozo wa uchangiaji wa hudama za afya Mipakani iliyotolewa na Wizara ya Afya. Kikao hicho kimefanyika tarehe 7 Machi, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Utalii, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Bw. Andrew Magombana, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Usafiri wa Barabara, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, amesema kuwa suala la afya ni mtambuka na linamuhusu kila Mtanzania, na kuwaasa wadau kuwa huru kuchangia mwongozo huo kwani suala la kulinda afya ya Watanzania ni muhimu.
“Leo tunakutana hapa kupitia maoni ya wadau yaliyotolewa tarehe 11 Disemba, 2024, ambayo yamechakatwa katika vikao mbalimbali na yamerudishwa kwetu ili tutoe maoni namna ya kuyaboresha kulingana na mahitaji ya Sekta ya Uchukuzi”, amesema Bw. Magombana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri Majini, Bw. Nelson Mlali, akzungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, amewakumbusha wadu hao kuitumia fursa hiyo kutoa maoni yenye mtazamo chanya ili kuboresha maeneo muhimu ya mwongozo huo.
“Suala ala uchangiaji wa huduma za afya ni la kisera linamgusa kila mtu katika mazingira mbalimbali. Ndio maana Wizara ya Afya imeona umuhimu wa kuwashirikisha wadau ili waone umuhimu wa kutoa maoni katika kuboresha mwongozo uliotolewa kwa kuzingatia kuwa Sekta ya Usafirishaji ndiyo inayoiunganisha nchi yetu na nchi nyingine kibiashara na kimahusiano. Aliwamba washiriki kutoa maoni yao hasa katika maeneo ya huduma zinazotakiwa kulipiwa, viwango vya tozo na mdau anayetakiwa kulipa tozo husika”, amesema Bw. Mlali.
Wadau wamepewa muda wa siku 14 kuendele kutoa maoni yao kuanzia tarehe 7 Machi, 2025.