Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa awahakikishia wananchi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, ujenzi wa bandari ya Lagosa kukamilika miezi sita ijayo.

Imewekwa: 13 October, 2023
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa awahakikishia wananchi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, ujenzi  wa bandari ya Lagosa kukamilika miezi sita ijayo.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) amewahakikishia wananchi wa vijiji vya mwambao wa Ziwa Tanganyika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, kuwa ujenzi wa mradi wa bandari ya Lagosa utakamilika kwa asilimia 100 katika muda wa miezi sita ijayo,  ujenzi huo utakapokamilika utafungua uchumi wa wananchi wa ukanda Kigoma kusini na kufanya biashara katika ukanda huo pamoja na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 Mhe. Mbarawa ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa bandari ya Lagosa tarehe 9  Oktoba, 2023.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Nelson Mlali amewashukuru wadau wa sekta ya usafiri wa maji wakiwemo Serikali za Mtaa, Beach Management Unit (BMU) na vyama vya wamiliki wa vyombo kwa jinsi wanavyoshirikiana na TASAC kudhibiti suala la usalama wa usafiri majini na kusajiri vyombo vyao kwa hiari.

TASAC  imeambatana na Mhe. Waziri wa Uchukuzi katika ziara hiyo iliyoanzia Mkoa wa Katavi katika bandari ya Karema na baadaye Mkoa wa Kigoma katika bandari ya Lagosa

Mrejesho, Malalamiko au Wazo