Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

WAZIRI ULEGA AIPONGEZA TASAC KWA WELEDI

Imewekwa: 28 January, 2025
WAZIRI ULEGA AIPONGEZA TASAC KWA WELEDI

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) ambalo ni mdhibiti wa usafiri wa majini nchini, kwa kufanya kazi kwa haraka na weledi katika kuhakikisha vivuko viwili vipya vya Sea Tax III na Sea Tax IV vinakaguliwa, kusajiliwa, na kupatiwa ruhusa ya kuanza shughuli zake. 

Mhe. Ulega ametoa pongezi hizo, leo terehe 23 Januari 2025 wakati akizindua vivuko hivyo vinavyomilikiwa na kampuni ya Azam Marine Co. Ltd katika hafla iliyofanyika katika eneo la Magogoni, ambapo vivuko hivyo vimeanza rasmi shughuli za kuvusha abiria kati ya maeneo ya Magogoni na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ulega ameongeza kuwa juhudi za TASAC zimeimarisha usalama wa usafiri wa majini nchini.

Aidha, Waziri Ulega amewataka Azam Marine Co. Ltd na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kuendelea kushirikiana kikamilifu katika kutekeleza jukumu la kuvusha watu katika eneo hilo, ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora, salama, na zenye ufanisi kwa wananchi.

Vivuko vya Sea Tax III na Sea Tax IV vinatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza msongamano wa usafiri ambao lilikuwa tatizo kubwa kwa eneo hilo la kwa kutoa huduma salama, ya haraka, na yenye viwango vya hali ya juu kwa wananchi wa Dar es Salaam.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo