WATUMISHI WA TASAC WAPATIWA MAFUNZO YA AFYA YA AKILI

Watumishi wa Idara ya Usalama, Ulinzi wa Vyombo vya Usafiri Majini na Utunzaji wa Mazingira Majini (DMSE), leo tarehe 20 Oktoba, 2025, wamepewa mafunzo ya Afya ya Akili ikiwa ni katika juhudi za taasisi katika kuhakikisha maafisa hao wanajiepusha na msongo wa mawazo na kuathiri utendaji kazi.
Mafunzo hayo yametolewa na Dokta Garvin Kweka, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa kikao kazi cha DMSE kinachofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere mjini Kibaha.
Katika kikao hicho watumishi hao watapata fursa ya kujipima na kujadili utendaji wao na kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji huo ikiwemo masuala ya Bajeti, vihatarishi pamoja na Mifumo ya Udhibiti Ubora wa huduma wanazotoa.
Kikao hicho kinafanyika kwa siku tano (5) kuanzia leo na kitamalizika tarehe 24 Oktoba, 2025.