Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Watumishi TASAC wapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya namna ya kutumia mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma

Imewekwa: 18 January, 2024
Watumishi TASAC wapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya namna ya kutumia mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma

Watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya namna ya kutumia mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi Katika Taasisi za Umma (Institution Performance Contract System- IPCS) tarehe 18 Disemba, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.

Wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Hamid Mbegu ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Shirika amewataka watumishi kuwa makini kufuatilia mafunzo hayo ili kupata uelewa wa mfumo huo.

 "Mafunzo haya ni nyenzo muhimu ya upimaji wa utendaji wa watumishi Serikalini, hivyo natoa rai kwa watumishi kuzingatia mafunzo haya ili kuweza kuelewa jinsi ya kutumia mfumo huu". Amesema Bw. Mbegu.

Mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Rais, Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kusimamiwa na Wizara ya Uchukuzi ambayo ni Wizara inayoisimamia TASAC. 

Serikali imewekeza kuboresha utendaji wa taasisi zake kwa kutumia mfumo wa kupima utendaji wa taasisi na watumishi na hii ni

Mrejesho, Malalamiko au Wazo