WATUMISHI TASAC WANOLEWA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI
WATUMISHI TASAC WANOLEWA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI
Imewekwa: 11 March, 2025

Watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 11 Machi, 2025 wamepatiwa mafunzo ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano katika Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo ni endelevu kwa watumishi wote wa TASAC na yanalenga kuwajengea uelewa na uwezo katika kuhakikisha wanajilinda na majanga pamoja na magonjwa wawapo katika utendaji kazi wa kila siku.