Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YATOA ELIMU YA USAFIRI MAJINI FUKWE YA MSIMBATI - MTWARA

Imewekwa: 10 February, 2026
TASAC YATOA ELIMU YA USAFIRI MAJINI FUKWE YA MSIMBATI - MTWARA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) tarehe 9 Februari, 2026 limetoa elimu ya usafiri kwa njia ya maji kwa wadau wake katika fukwe ya Msimbati, mkoani Mtwara. 

Elimu hiyo imelenga kuongeza uelewa kuhusu matumizi salama ya vyombo vya usafiri majini, ikiwemo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama wakati wa safari.

Katika utoaji wa elimu hiyo, maafisa wa TASAC wamewakumbusha wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya usafiri majini, wavuvi pamoja na abiria umuhimu wa kuvaa vifaa vya kujikinga kama vile jaketi za kuokoa Maisha (life jacket), kufanya ukaguzi wa vyombo kabla ya safari na kuepuka kupakia abiria au mizigo kupita kiasi. 

Wadau walioshiriki wamepongeza juhudi za TASAC kwa kuendelea kuwafikia moja kwa moja katika maeneo yao ya kazi na kutoa elimu yenye tija. Wamesema elimu hiyo itasaidia kupunguza ajali za majini na kuongeza usalama wa vyombo na watumiaji wake, huku wakiahidi kushirikiana na TASAC katika kutekeleza miongozo ya usalama kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Elimu kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira Majini mkoani Mtwara imeanza tarehe 9 Februari, 2026 na itaendelea hadi tarehe 13 Februari, 2026.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo