Wafanyakazi wanawake wa TASAC wajumuika na Wanawake walio katika sekta ya usafiri Majini (Women in Maritime) kuwatembelea wafungwa wanawake waliopo Chuo cha Mafunzo visiwani Zanzibar
Wafanyakazi wanawake wa TASAC wajumuika na Wanawake walio katika sekta ya usafiri Majini (Women in Maritime) kuwatembelea wafungwa wanawake waliopo Chuo cha Mafunzo visiwani Zanzibar
Imewekwa: 20 May, 2024
Katika kuendeleza Maadhimisho ya Siku ya Wanawake walio katika sekta ya usafiri Majini (Women in Maritime), Umoja wa wanawake walio katika sekta ya Usafiri Majini katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) leo tarehe 19 Mei, 2024 inaendelea kuigusa jamii kwa kufanya shughuli mbali mbali kwa kuwatembelea wafungwa wanawake waliopo Chuo cha Mafunzo visiwani Zanzibar na kutoa misaada mbali mbali.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake walio katika sekta ya Usafiri Majini yameanza jana tarehe 18 Mei, 2024, na yataendelea hadi tarehe 20 Mei, 2024 ambapo wataendelea kufanya shughuli mbalimbali kwenye jamii