Wafanyakazi wa TASAC washiriki Bonanza la Michezo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TASAC Bw. Nahson Sigalla ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi TASAC, ameongoza Wafanyakazi wa TASAC katika Bonanza la Michezo liliofanyika katika fukwe za Jangwani Sea Breeze Resort jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni, 2024
Bonanza hilo lililohisisha michezo mbalimbali kama, mpira wa miguu, mpira wa kikapu, karata, bao, mbio, kuogelea, kukimbiza kuku, kuvuta kamba nk. limeandaliwa kwa lengo la kujiweka sawa kiafya lakini pia kudumisha umoja na mshikamano nje ya eneo la kazi.
Akizungumza katika katika bonanza hilo Bw. Sigalla amewapongeza wafanyakazi wa TASAC kwa kujitokeza katika bonanza hilo lakini pia kwa kamati ya maandalizi kwa kuwezesha kufanikisha bonanza hilo.
Aidha, Bw. Sigalla ametoa wito kwa wafanyakazi wa TASAC na wananchi kwa ujumla kuzingatia michezo kwa sababu ina faida nyingi katika mwili lakini pia inadumisha ushirikiano mzuri hata nje ya kazi.