Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Wafanyakazi wa TASAC wapewa mafunzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Imewekwa: 29 May, 2024
Wafanyakazi wa TASAC wapewa mafunzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Mafunzo ya Usalama na Afya mahali pa kazi, yametolewa leo tarehe 28 Mei,2024 kwa wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika ukumbi wa Chuo cha Utalii cha  Dar es salaam kilichopo jijini Dar es sam.  Mwakilishia kutoka Wakala wa Usalama na Afya  Mahala pa Kazi (OSHA) ametoa mafunzo hayo yaliyohusu masuala  mbalimbali ya Usalama na Afya Mahala pa kazi.

Mafunzo hayo yamejikita katika kuainisha Sheria na Kanuni mbalimbali zinazosimamiwa na OSHA katika maeneo ya kazi ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari kwa lengo la kuwa salama wakati wa kutekeleza majukumu mahala pa kazi.

Aidha, semina hiyo ambayo ni endelevu inatarajia kuleta mabadiliko na kutambua vihatarishi vilivyopo, namna ya kuvidhibiti pamoja na kukabiliana navyo pale inapotokea tatizo bila kuathiri utendaji kazi wa kila siku.

Mafunzo hayo ni ya siku mbili yatahimishwa kesho  Jumatano tarehe 29 Mei, 2024.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo