Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

WADAU WATEMBELEA BANDA LA TASAC MAONESHO YA OSHA

Imewekwa: 28 April, 2025
WADAU WATEMBELEA BANDA LA TASAC MAONESHO YA OSHA

Wadau mbalimbali wametembelea Banda la Shirikia la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika maonesho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) yanayofanyika Mkoani Singida.

Wadau hao wametembelea banda hilo leo tarehe 24 Aprili, 2025 katika viwanja vya Mandewa mjini Singida na wamejifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAC, ikiwemo juhudi zinazofanywa na Shirika katika kuhakikisha usimamizi wa masuala ya usalama na afya kwa watumishi na wadau mbalimbali.

Moja ya wadau waliotembelea banda hilo ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mabaharia Tanzania (TASU), Bw. Hatibu Omary Mohamed ambapo amepongeza juhudi za TASAC katika kusimamia mabaharia hapa nchini.

TASAC ni moja ya taasisi zinazoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya OSHA yenye kauli mbiu “ Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidijitali katika kuimarisha Usalama na Afya Mahali Pa Kazi ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mnamo tarehe 30 Aprili, 2025

Mrejesho, Malalamiko au Wazo