Wadau Vyombo vidogo waaswa kuzingatia masharti.
Katibu Tawala wa mkoa wa Geita, Bwana Mohammed Gobani amewataka watoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo mkoa wa Geita, Kagera na Mwanza kuzingatia kanuni na mashariti ya leseni wanazopewa na TASAC katika kutoa huduma ya usafirishaji ziwa Victoria. Ameyasema hayo, wakati akifungua warsha ya kuelimisha wamiliki, wasafirishaji, wavuvi na wasimizi wa mialo (BMU) siku ya Ijumaa tarehe 19/01/2024 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu Mkoa wa Geita. Bwana Mohammed Gobani alisema, "Tumekutana hapa kujadiliana na kuelimishana na kuboresha huduma ya usafiri majini ili iwe salama na shirikishi kwa wadau wote wa ziwa Victoria. Mnatakiwa kuvaa maboya, kusafiri mchana, kuacha taarifa za safari yako katika mwalo rasmi ambao umeondoka. Haya ni ya lazima kuyafuata ili kulinda uhai wa maisha yetu wakati tunapofanya shughuli mbalimbali ziwani".