Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

USHIRIKISHWAJI WADAU MUHIMU KWA KANUNI BORA

Imewekwa: 09 September, 2024
USHIRIKISHWAJI WADAU MUHIMU KWA KANUNI BORA

Shirika la Uwakala Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 9 Septemba 2024 limefanya kikao cha kupokea maoni ya wadau juu Rasimu ya Kanuni za Biashara za Meli kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa  Chuo cha Utalii, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa  ufunguzi wa kikao hicho, Bw. Biseko Chiganga kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi  amesema wadau sekta ya uchukuzi wanahitaji  kushirikiana kupitia majadiliano ya pamoja hili kuweza kuboresha sekta nzima ya uchukuzi hapa nchini.

Bw. Chiganga amesema kuwa nia ya Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ili kufanya huduma za biashara za meli kuwa na mazingira rafiki na kukidhi mahitaji ya sasa na baadae ya sekta ndogo ya usafirishaji majini.

"Kikao hiki ni daraja muhimu la kutengeneza kanuni bora na zenye tija kwa makundi yote yanayohusika. Hivyo ni matumaini yangu kuwa mtatoa maoni na mapendekezo yatayosaidia kuboresha rasimu hii ili ikidhi mahitaji ya sasa na baadae ya usafirishaji majini ili kuwa na mazingira rafiki," amesema Bw. Chiganga.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TASAC, Bi. Judithi Kakongwe ambaye alikuwa akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, amesema kuwa Kanuni ya Huduma ya Biashara imefutwa baada ya Serikali kufanya mabadiliko ya Sheria ya Fedha Na. 5 ya Mwaka 2022 na kupelekea Kanuni ya Huduma za Biashara ya Meli kuhitaji mabadiliko mengi, hivyo kulazimu kanuni hiyo kutungwa upya.

Kwa mujibu wa Sheria, TASAC inatakiwa kukusanya maoni kila inapofanya mabadiliko ya kanuni au sheria ili kufanya kanuni hizo ziweze kutekelezwa na kuwa na ufanisi. 

Mnamo, mwezi Agosti, 2024 TASAC ilifanya mkutano wa wadau ili kukusanya maoni ya maboresho ya kanuni ya mabadiliko ya kanuni za kushughulikia malalamiko ya mwaka 2018.

Wadau wanaweza kuwasilisha maoni yao kwenda TASAC kwa njia ya maandishi ndani ya muda wa kwa siku kumi na nne (14) kuanzia leo tarehe, 9 Septemba, 2024 kupitia barua pepe dg@tasac.go.tz.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo