Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

US COAST GUARD WAHITIMISHA ZIARA YAO

Imewekwa: 28 February, 2025
US COAST GUARD WAHITIMISHA ZIARA YAO

Ujumbe maalum wa Kikosi cha Ulinzi wa Pwani ya Marekani (US Coast Guard), leo tarehe 28 Februari, 2025 wamehitimisha ziara yao kwa kukutana na timu ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), katika Makao Makuu ya TASAC, jijini Dar es Salaam.

Wakiwa katika ofisi za TASAC, walipokelewa na Mkurugenzi wa Udhibiti, Usalama,Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira ya  Majini, Wakili Leticia Mutaki pamoja na wageni wamejadili masuala mbalimbali yaliyotokana na ziara hiyo hapa nchini.

Ujumbe huo umeahidi kufanyia kazi yote yaliyojadiliwa kwenye kikao cha kwanza na TASAC ikiwemo kushirikiana katika kutoa mafunzo ya kukabiliana na uhalifu wa kimtandao.

Wakiwa nchini, pia walipata fursa kutembelea Bandari za Dar es Salaam na Malindi Zanzibar pamoja na Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokoaji (MRCC) kilichopo jijni Dar es Salaam.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo