Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

UJUMBE WA TANZANIA NA LIBERIA WAKUTANA LONDON KUJADILI USHIRIKIANO WA BAHARINI

Imewekwa: 27 November, 2025
UJUMBE WA TANZANIA NA LIBERIA WAKUTANA LONDON KUJADILI USHIRIKIANO WA BAHARINI

Ujumbe wa Tanzania, leo tarehe 26 Novemba 2025, umekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Liberia pembezoni mwa Mkutano wa 34 wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) unaoendelea jijini London, nchini Uingereza.

Mazungumzo hayo yamelenga kuanzisha ushirikiano mpya kati ya nchi hizo mbili katika masuala ya usimamizi wa usafiri wa majini, hususan usajili wa meli na kutambuliana vyeti vya mabaharia.

Katika mazungumzo hayo, Ujumbe wa Liberia umeonesha dhamira ya kufanya ziara nchini Tanzania mwishoni mwa Januari 2026 kwa ajili ya kusaini hati za makubaliano (MoUs) jijini Dar es Salaam.

Ushirikiano huu unatarajiwa kufungua fursa zaidi kwa mabaharia wa Tanzania kufanya kazi katika meli zilizosajiliwa Liberia, pamoja na kutoa msukumo katika kuboresha usajili wa meli za Tanzania, kuongeza ushindani wake kwenye soko la kimataifa na kuimarisha huduma za baharini.

Liberia ni nchi ya pili duniani iliyosajili na kumiliki meli nyingi zaidi duniani pamoja na kuwa na rejista kubwa na kongwe zaidi kimataifa. Nchi hiyo inachangia sehemu kubwa ya meli zinazofanya biashara duniani kupitia mfumo wake wa usajili wa meli wa masharti nafuu (open registry), ambao umekuwa kivutio kwa waendeshaji wa meli kutokana na ufanisi, viwango vya kimataifa na mazingira wezeshi ya utoaji huduma.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo