Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TPA Tanga yapewa kongole na TASAC

Imewekwa: 13 August, 2024
TPA Tanga yapewa kongole na TASAC

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania -TASAC imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa  kutekeleza vema mradi wa uboreshaji wa bandari  ya Tanga na kuwezesha meli kufunga ghatini na kuongeza asilimia 30 ya mapato ya bandari ya Tanga.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Bodi hiyo Nahodha Mussa Mandia wakati akizungumza na vyombo vya habari tarehe 26 Julai, 2024 jijini Tanga ambayo ni siku ya tano tangu bodi hiyo ianze ziara ya ukaguzi wa huduma ya udhibiti zinazofanywa na TASAC.

"Tumevutiwa  na utaratibu wa usalama.wa bandari wenye kiwango  cha usalama.daraja la kwanza ambavyo ni vigezo vya  bandari inayotoa huduma kwa viwango vya kimataifa.Pili tumeona mazingira safi ya bandari na shughuli zinaendeshwa kwa mpangilio mzuri.Tuna kila sababu ya kujivunia utendaji wenu wa kazi na uwekezaji wa Serikali awamu ya Sita inayoongozwana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe, Dkt.Samia Suluhu Hassan na kusababisha mapato kuongezeka kwa asilimia 30.Hongera sana uongozi TPA na bandari ya Tanga." Amesema Nahodha Mussa Mandia.

Bandari ya Tanga ilijengwa tangu mwaka 1888 na mwazo ilikuwa inatoa huduma kwa mzigo kushusha kwenye baji umbali kilomita 1.7 na kukotwa hadi ghatini.Lakini kwa sasa mara baada ya kuboresha meli inakuja moja kwa moja na kufunga ghatini.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Nahodha Mussa Mandia amewaasa uongozi wa bandari Tanga kutenga eneo la mizigo michafu na safi, kuendelea ujenzi bandari katika eneo la zaidi mitaa 300 kwa ajili ya kuwa na ghati ya kuhudumia meli au boti za abiria pasipokuingilia na shughuli za ghati zinazohusika kushusha mizigo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bwana Mohamed Salum  ametoa wito kwa bandari kutenganisha eneo la mizigo hatarishi na mizigo mengine. Pia ametoa wito kwa mawakala wa meli kuanza kuleta meli bandari ya Tanga kwa mizigo inapakuliwa kwa haraka na gharama.nafuu ukilinganisha na zamani walipokuwa wanatumia baji.

Aidha ameongeza bandari iendelee kufanya maboresho na watoa huduma za uwakala wa forodha, wapakiaji mizigo wawe eneo la kufanyia kazi nje ya bandari ili kuongeza ufanisi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo