Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YAWATEMBELEA NA KUWASIKILIZA WADAU WA SEKTA YA MADINI GEITA

Imewekwa: 23 September, 2025
TASAC YAWATEMBELEA NA KUWASIKILIZA WADAU WA SEKTA YA MADINI GEITA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini Geita limekutana na wadau wa sekta ya madini na kuwapa elimu ya majukumu ya kipekee inayotekeleza. 

Timu ya Maafisa wa TASAC ikiongozwa na Bw. Gracian Mutabuzi, Afisa Mwandamizi wa Ugomboaji, imetembelea kwenye mabanda ya wateja hao pamoja na wale waliofika kwenye Banda la TASAC na kusikiliza maoni yao yatakayosaidia  kuboresha huduma za TASAC na kujenga uhusiano chanya kati yao na wateja tunaowahudumia.

Bw. Mutabuzi amesema kuwa mteja anapoingiza kemikali nchini au akiwa na makinikia anapaswa kuwasilisha nyaraka zake kwenye mfumo wa TASAC kwa njia ya mtandao ili kuweza kufanyiwa kazi.

Baadhi ya wateja waliotembelewa ambao ni pamoja na GGM, JEMA na Mkemia Mkuu wa Serikali wamesema wamefurahishwa na kazi zinazofanywa na TASAC katika kuhudumia ugomboaji wa bidhaa maalum ikiwemo makinikia, silaha na vilipuzi, kemikali, nyara za Serikali na Wanyama hai.

Maonesho hayo yanafanyika katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita yalianza rasmi  tarehe 18 Septemba, 2025 yatafika tamati tarehe 28 Septemba, 2025,yana kauli mbiu "Ukuaji wa Sekta ya Madini ni Matokeo ya Matumizi ya Teknolojia Sahihi na Uongozi Bora, Shiriki Uchaguzi Mkuu  2025".

Mrejesho, Malalamiko au Wazo