Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YAWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI WAKE KUHUSU UADILIFU NA RUSHWA

Imewekwa: 07 October, 2025
TASAC YAWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI WAKE KUHUSU UADILIFU NA RUSHWA

Watumishi kutoka idara kuu za Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 06 Oktoba, 2025 wamepewa Mafunzo ya Uadilifu na Rushwa ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mpango Kazi wake.

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum amesema kwamba mafunzo hayo hayapaswi kuonekana kama wajibu tu, bali kama fursa ya kujithamini na kuongeza maarifa. 

Bw. Salum amewaelekeza wafanyakazi hao kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ili yawe na matokeo chanya katika maeneo yao ya kazi.

“Ni matarajio yangu baada ya mafunzo haya  tutashuhudia kuimarika kwa uadilifu na uwajibikaji kwa watumishi, uzingatiaji wa kanuni za maadili ya utumishi wa umma, ulinzi wa taarifa za Serikali na siri za taasisi pamoja na kuimarika kwa imani ya wadau kwa TASAC kama taasisi ya kuigwa katika uadilifu na weledi,” amesema Bw. Salum.

Amewataka watumishi hao kuwa mabalozi wazuri katika Shirika na jamii ili kujenga utumishi uliotukuka na kukuza imani ya wananchi wote.

Mafunzo hayo yanafafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 06 hadi 07 Oktoba, 2025 yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu madhara ya rushwa, njia za kuepuka na wajibu wao kama watumishi wa umma katika kulinda heshima na uaminifu kwa Shirika ambapo mada mbalimbali zinatolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Ofisi ya Rais.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo