Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yawajengea uelewa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini

Imewekwa: 13 August, 2024
TASAC yawajengea uelewa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini

Shilika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo tarehe 23 Julai, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo SUMATRA house jijini Dar es Salaam limekutana na kutoa elimu kwa vijana kutoka vyuo mbalimbali kupitia Shirika lisilo la Kiserikali linalojulikana kama “Munutual Generation International (MGI)” linalojihusisha na kutoa elimu ya kujitegemea kwa vijana ili kuweza kutambua fursa za ajira zinazowazunguka ili kujikwamua kiuchumi. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Shirika (DCS) Bi. Pili Mazowea ambaye ni Meneja Rasilimali watu na Utawala amefungua kikao hicho na kuwaeleza wanavyuo hao kuwa TASAC ipo tayari muda wote kutoa elimu na kueleza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya usafiri majini kwani wanavyuo ni wadau muhimu katika sekta hii.

Aidha, mada mbalimbali zimewasilishwa kutoka Kurugenzi ya Usalama,Ulinzi wa Vyombo vya Usafiri Majini na Utunzji wa Mazingira (DMSE), Kurugenzi ya Huduma za Udhibiti wa Usafiri Majini (DMTR), Kurugenzi ya Huduma za Biashara za Meli (DSB), Kurugenzi ya Udhibiti Uchumi (DER) na Kitengo cha Huduma za Sheria (DLS). 

Wanafunzi hao wametoka katika vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo cha Kimataifa cha Kampala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha ARDHI, Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) na Chuo cha Biashara (CBE)

Mrejesho, Malalamiko au Wazo