Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YATUNUKIWA TUZO KWA KUWEZESHA WIKI YA USAFIRI ENDELEVU ARDHINI 2025

Imewekwa: 27 November, 2025
TASAC YATUNUKIWA TUZO KWA KUWEZESHA WIKI YA USAFIRI ENDELEVU ARDHINI 2025

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetunukiwa tuzo maalum kwa mchango wake mkubwa katika kudhamini na kuwezesha Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini 2025, yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo leo Novemba 26, 2025, umeongozwa na Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Mchemba, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC). 

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, tuzo hiyo imepokelewa na Bw. Hamid Mbegu, Mkurugenzi wa Huduma za Shirika, ambaye amesema kuwa TASAC itaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine kuendeleza usafiri salama, endelevu na wenye tija kwa uchumi wa taifa. Aidha, kuendelea kutekeleza Maelekezo ya Mheshimiwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano kuhusu kuunganisha pamoja njia zote za Usafiri ili kuleta Tija na Ufanisi (Intermodal Transport).

Bw. Mbegu ameongeza kuwa ushiriki wa TASAC kwenye maadhimisho haya ni sehemu ya jitihada endelevu za shirika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa usafiri majini katika biashara, usalama na uhifadhi wa mazingira.

Tuzo iliyokabidhiwa TASAC imetolewa kutambua mchango wake kama mdhamini muhimu wa maadhimisho hayo, pamoja na juhudi zake zinazolenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu usalama, ulinzi na udhibiti wa ubora katika sekta ya usafiri majini, ambayo inabeba nafasi muhimu katika kukuza uchumi wa buluu na kuimarisha usafiri endelevu.

Kupitia tuzo hii, TASAC inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama mdau muhimu katika kukuza usafiri endelevu na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya uchukuzi nchini.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo