TASAC YATOA ELIMU MAONESHO YA MADINI
TASAC YATOA ELIMU MAONESHO YA MADINI
Imewekwa: 04 October, 2024
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) linaendea kutoa elimu kuhusu majukumu inayoyatekeleza ikiwemo masuala ya usalama, ulinzi pamoja na utunzaji wa mazingira ya usafiri kwa njia ya maji kwa wadau mbalimbali wa Mkoa wa Geita na viunga vyake.
TASAC ni moja ya taasisi zinazoshiriki katika Maonesho ya 7 ya Teknolojia na Madini yanayofanyika Mkoani Geita katika Viwanja vya Bombambili.
Maonesho hayo yameanza tarehe 02 Oktoba, 2024 na yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 13 Oktoba, 2024, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.