TASAC yatoa elimu kwa wadau Visiwani Zanzibar
TASAC yatoa elimu kwa wadau Visiwani Zanzibar
Imewekwa: 19 January, 2024
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki kutoa elimu kwa wadau katika maonesho ya kumbukizi ya miaka 60 ya Mapinduzi matukufu visiwani Zanzibar .
Maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya maonesho Fumba, yameanza tarehe 8- 14 Januari, 2024 ambapo yamefunguliwa Rasmi tarehe 10 Januari, 2024 na Mgeni Rasmi Mhe. Hussein Mwinyi, Rais na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Tunaunganisha. Tunakutanisha. Tunakuza.
TASAC imetoa elimu ya Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira pamoja na Majukumu yanayo tekelezwa kwa Mujibu wa Sheria.
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania linawakaribisha kutembelea banda la TASAC ili kupata elimu kuhusu usafiri bora na salama kwa njia ya maji.