Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YATOA ELIMU KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FIATA-RAME

Imewekwa: 05 May, 2025
TASAC YATOA ELIMU KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FIATA-RAME

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendelea kutoka elimu kuhusu majukumu yake katika Maonesho ya Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Vyama vya Mawakala wa Ushuru wa Forodha kwa upande wa Afrika Mashariki na Kati (FIATA-RAME) uliokuwa unafanyika katika Viwanja vya Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar.

 

TASAC ni moja ya taasisi zinazoshiriki maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi tarehe 30 Aprili, 2025 na Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri majini hususan Mawakala wa Ushuru wa Forodha kwa kutoka Afrika Mashariki na Kati.

 

Mkutano huo ulifungwa rasmi tarehe 01 Mei, 2025 na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Bandari Zanzibar, Bw. Akif Ali Khamis, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum leo.

 

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano huo, Bw. Khamis amesema kuwa wadau wanatakiwa kuwa na dhamira ya pamoja katika kujenga ushirikiano unaovuka mipaka ili kendeleza sekta ya usafiri majini hasa miundombinu ya bandari ili iendane na maendeleo ya kisasa na kuimarisha usafiri endelevu.

 

"Ni lazima tuwe chachu ya mabadiliko tunayoyatamani kuyaona kwa ajili ya mataifa yetu, kanda zetu, dunia nzima, na kwa vizazi vijavyo kwa kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya bandari ya kisasa," alisema Bw. Khamis.

 

Kaulimbiu ya mkutano huu ilikuwa: “Ushirikiano katika Uchumi wa Buluu: Kubadilisha Sekta ya Usafirishaji na Uchukuzi kwa Maendeleo Endelevu.”

Mrejesho, Malalamiko au Wazo