Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YATOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA USAFIRI ENDELEVU ARDHINI

Imewekwa: 26 November, 2025
TASAC YATOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA USAFIRI ENDELEVU ARDHINI

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendelea kutoka elimu kuhusu majukumu yake katika Maonesho ya Usafiri Endelevu ardhini yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wametembelea Banda la TASAC na kupata elimu ya usalama, ulinzi wa vyombo vya usafiri majini na utunzaji wa mazingira majini, lakini pia shughuli za usafiri majini kwa ujumla.

TASAC imekuwa ikitumia fursa ya maonesho mbalimbali kutoa elimu ya umuhimu wa huduma za usafirishaji majini, usalama wa vyombo vya usafiri majini, pamoja na fursa za biashara zinazopatikana kupitia sekta ya usafiri kwa njia ya maji.

Wadau waliotembelea banda hilo wamepongeza jitihada za Shirika katika kuelimisha Umma na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia usafirishaji wa majini.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu Nishati safi na ubunifu katika usafirishaji yalianza rasmi  tarehe  24 Novemba, 2025 na yatafika tamati tarehe 29 Novemba, 2025.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo