Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YASHIRIKIANA NA KAMATI YA AMANI MKOA WA DAR ES SALAAM KUFADHILI DUA YA KUMUOMBEA MHESHIMIWA RAIS KUADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA

Imewekwa: 28 January, 2025
TASAC YASHIRIKIANA NA KAMATI YA AMANI MKOA WA DAR ES SALAAM KUFADHILI DUA YA KUMUOMBEA MHESHIMIWA RAIS KUADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefadhili dua maalum katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika tarehe 27 Januari, 2025 katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Dua hiyo iliongozwa na viongozi mbalimbali wa dini akiwepo Mchungaji Boniface Mwamposa, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, na Kiongozi wa Kanisa la Agape, Dkt. Vernon Fernandes ambapo walitumia fursa ya dua hiyo kuwataka Watanzania kuilinda na kuidumisha amani iliyopo nchini.

Pamoja na dua hiyo, kulikua na keki maalum iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ilikatwa ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya siku hii.

Dua hiyo iliandaliwa na Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya Mama Samia Support na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka sekta ya umma na sekta binafsi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo