TASAC yashiriki Tamasha la Maandalizi ya Maonesho ya Biashara Kati ya Tanzania na India (INDO TANZANIA INTERNATIONAL EXPO)
TASAC yashiriki Tamasha la Maandalizi ya Maonesho ya Biashara Kati ya Tanzania na India (INDO TANZANIA INTERNATIONAL EXPO)
Imewekwa: 14 June, 2024
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni moja ya Taasisi zinazoshiriki katika Tamasha la Maandalizi ya Maonesho ya Biashara Kati ya Tanzania na India (INDO TANZANIA INTERNATIONAL EXPO) katika Viwanja vya Stendi tarajiwa ya Mabasi ya Kusini (Dkt Samia Suluhu Hassan Bus Terminal), Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Maonesho hayo yameandaliwa na Shirikisho la vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) kwa Lengo la kukutanisha taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi pamoja vyama vya ushirika na wadau kwa ujumla ili kuweza kutoa elimu juu ya shughuli zao.
Maonesho hayo yameanza tarehe 10 Juni, 2024 na yanatarajia kuhutimishwa tarehe 16 Juni, 2024.