TASAC YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
TASAC YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Imewekwa: 17 June, 2025

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) linashiriki maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo tarehe 16 Juni 2025 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kitaifa ni: "Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na kuchagiza Uwajibikaji".
Maonesho hayo yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 23 Juni, 2025.