TASAC yashiriki Maonesho ya Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
TASAC yashiriki Maonesho ya Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
Imewekwa: 13 August, 2024
Wadau mbalimbali wa Usafiri Majini wametembelea Banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho ya Kilimo maarufu kama Nane Nane tarehe 04 Agosti, 2024 katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Kauli mbiu ya maonesho haya mwaka huu ni "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi"
Maonesho hayo yameanza rasmi tarehe 01 Agosti, 2024 na yatahitimishwa tarehe 08 Agosti, 2024.