Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yashiriki Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma

Imewekwa: 18 June, 2024
TASAC yashiriki Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni moja ya Taasisi zinazoshiriki katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.

Maonesho hayo yameandaliwa kwa lengo la kukutanisha taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, vyama vya ushirika na wadau kwa ujumla ili kuweza kutoa elimu juu ya shughuli mbalimbali wanazozifanya.

Maonesho hayo yameanza tarehe 16 Juni, 2024 na yanatarajia kuhitimishwa tarehe 23 Juni, 2024.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo