Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yashiriki katika kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika Viwanja vya "General tyre" jijini Arusha.

Imewekwa: 08 May, 2024
TASAC yashiriki katika kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika Viwanja vya "General tyre" jijini Arusha.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizoshiriki maonesho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi yanayoratibiwa na  OSHA katika viwanja vya "General tyre", jijini Arusha.

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Doto Biteko, amewaongoza mamia ya wafanyakazi nchini kuadhimisha siku hii tarehe 28 Aprili, 2024.

Akihutubia ameeleza kuwa jukumu la msingi la OSHA ni kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya nchi inalindwa na maeneo ya kazi yanakuwa na uzalishaji endelevu.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi katika Usalama na Afya Kazini, Sajili Eneo la Kazi OSHA katika harakati za kupunguza Athari hizo".
TASAC  ni mojawapo ya taasisi zinazoshiriki maadhimisho haya.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo