WADAU MBALIMBALI WATEMBELEA TASAC KATIKA MAONESHO YA SABASABA
WADAU MBALIMBALI WATEMBELEA TASAC KATIKA MAONESHO YA SABASABA
Imewekwa: 01 July, 2026
Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba) yanayoendelea katika Viwanja vya SabaSaba, Dar es Salaam, kwa lengo la kupata elimu kuhusu usafiri kwa njia ya maji pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.
Kupitia maonesho hayo, TASAC inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ya kusimamia usalama, ulinzi na ubora wa huduma za usafiri kwa njia ya maji, sambamba na kuhamasisha matumizi salama ya vyombo vya usafiri majini.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu “Hii Kubwa Kuliko” yalianza rasmi tarehe 28 Juni na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai, 2026.