Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YASHIRIKI NA KUDHAMINI KONGAMANO LA PILI LA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI

Imewekwa: 23 July, 2026
TASAC YASHIRIKI NA KUDHAMINI KONGAMANO LA PILI LA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki na kuwa miongoni mwa wadhamini wa Kongamano la Pili la Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), lililofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 21 hadi 22 Julai 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Kongamano hilo lilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, na kuwakutanisha viongozi wa Serikali, wataalamu wa ulinzi na usalama, wanazuoni pamoja na wadau kutoka sekta mbalimbali kujadili masuala ya kimkakati yanayohusu ulinzi, usalama na maendeleo endelevu ya Taifa.

Kupitia udhamini huo, TASAC inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na majukwaa yanayochochea mijadala ya kisera, tafiti, ubunifu na ushirikiano wa kimkakati unaochangia kuimarisha ulinzi na usalama katika sekta ya usafiri majini, na kukuza biashara, uchumi wa buluu na maendeleo ya Taifa

Mrejesho, Malalamiko au Wazo