TASAC yashiriki hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti ya doria ya kukabiliana na uhalifu katika bahari na maziwa makuu
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizoshiriki katika hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti ya doria ya kukabiliana na uhalifu katika bahari na maziwa makuu.
Hafla hiyo imefanyika katika Bandari ya Dar es Salaam tarehe 21 Aprili, 2024 na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wanaojihusisha na shughuli za majini ikiwemo Wizara ya Ulinzi na Usalama, Wizara ya Uvuvi, Mamlaka ya Bandari-TPA pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Jeshi la Wanamaji.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo aliwataka wadau wote ambao watatumia boti hiyo kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha boti hiyo inafanya kazi kama ilivyokusudiwa katika kupambana na vitendo viovu vinavyofanyika katika bahari na maziwa makuu ikiwemo uvuvi haramu.
TASAC imewakilishwa na Naho. Musa Mandia ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Mohammed Salum.