Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yapata mafunzo maalum ya kukabiliana na changamoto za Ulinzi, Usalama na Usimamizi wa Usafiri majini

Imewekwa: 18 January, 2024
TASAC yapata mafunzo maalum ya kukabiliana na changamoto za Ulinzi, Usalama na Usimamizi wa Usafiri majini

Mkurugenzi wa Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira ya Usafiri kwa Njia ya Maji  kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bi. Leticia Mutaki ameishukuru Serikali ya Uingereza kupitia Idara ya Uchukuzi kwa kutoa mafunzo maalum ya  kukabiliana na changamoto za Ulinzi, Usalama na Usimamizi wa usafiri wa majini kwa taasisi za Serikali nchini.
 
Bi. Mutaki amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani ukuaji wa teknolojia katika usimamizi na uboreshaji wa miundombinu ya usafiri majini umeongeza viashiria vya changamoto za majanga hivyo ni muhimu kwa taasisi hizo kuandaa mpango maalum utakaoainisha jukumu la kila taasisi hususani wakati wa majanga.
 
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kufunga mafunzo hayo Bi. Mutaki amewataka wadau kuhakikisha wanafanya kwa vitendo kile walichofundishwa ili kuimarisha usimamizi na utendaji katika usafiri majini.
 
“Mafunzo haya tuliyopata ni muhimu sana kwetu sababu yatatusaidia kuweka mikakati ya pamoja na kuwa na mpango mkakati utakaohusisha kila mdau.'' Ameongezea Bi. Mutaki.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo