TASAC YANG’ARA TUZO ZA UANDAAJI WA TAARIFA YA MAHESABU KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeshika nafasi ya kwanza katika tuzo ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa mwaka 2023 kati ya Mamlaka 9 za Udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini.
Tuzo hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, CPA Benjamin Mashauri ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 29 Novemba, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imepokelewa na CPA Pascal Kalomba Mkurugenzi wa Fedha kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum.
TASAC imeshika nafasi ya kwanza kwa mara ya tatu mfululizo, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2021, mara pili mwaka 2022 na mara tatu kwa mwaka 2023.
Kwa mwaka 2023, jumla ya taasisi 86 za Serikali na sekta binafsi katika maeneo wanayothibiti zimeshindishwa.