TASAC YANG’ARA KATIKA TUZO ZA UANDAAJI WA TAARIFA ZA MAHESABU KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeibuka kinara kwa kushika nafasi ya pili katika Tuzo za Uandaaji wa Taarifa za Mahesabu kwa Viwango vya Kimataifa, zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Tuzo hiyo imepokelewa na CPA Pascal Karomba, Mkurugenzi wa Fedha wa TASAC, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, katika hafla iliyofanyika tarehe 4 Desemba 2025, katika Ukumbi wa Hoteli ya APC, Bunju jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hizo, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratias Rusetura (Mb) aliyemwakilisha Waziri wa Fedha alisema kuwa taarifa za mahesabu zilizoandaliwa kwa viwango sahihi ni msingi muhimu wa maendeleo ya taasisi na uchumi wa taifa.
“Taarifa hizi za mahesabu ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa taasisi na taifa kwa ujumla,” amesema Mhe. Rusetura.
TASAC kupata tuzo hiyo kunadhihirisha dhamira ya Shirika katika kuimarisha usimamizi wa fedha, uwazi, na uwajibikaji kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa taarifa za kifedha.