TASAC YAKUTANISHA WADAU WA USAFIRISHAJI MAJINI
TASAC YAKUTANISHA WADAU WA USAFIRISHAJI MAJINI
Imewekwa: 11 September, 2025

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo tarehe 8 Septemba, 2025 limekutanisha wadau wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji kwenye ofisi za TASAC zilizopo jengo la Golden Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Dhumuni la kikao hicho ni kujadili changamoto za ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam baada ya baadhi ya watoa huduma kupeleka maombi hayo TASAC.
Taasisi zilizohudhuria kikao hicho ni Mamlaka ya Bandari (TPA), TASAA, DP WORLD na TEAGL ambapo wote kwa pamoja walikubaliana kutatua changamoto hizo kwa haraka ili kuongeza ufanisi wa Bandari zetu nchini.
Katika kikao hicho, changamoto zilizojadiliwa ni utaratibu wa uingizaji meli bandarini pamoja na namna ya upakiaji wa meli za mizigo mchanganyiko.