Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YAKUTANA NA WADAU KUPOKEA MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA KANUNI MBALIMBALI

Imewekwa: 29 May, 2023
TASAC YAKUTANA NA WADAU KUPOKEA MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA KANUNI MBALIMBALI

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekutana na wadau katika mkutano wa uwasilishaji mapendekezo ya marekebisho ya kanuni mbalimbali na upokeaji wa maoni ya wadau.

Kanuni hizo ni Kanuni za Miundombinu ya Kupokea Taka Bandarini, Kuzuia Uchafu Utokanao na Meli (The Merchant Shipping Agencies), Port Waste Reception Facilities) , Regulation 2023 na Marekebisho ya Kanuni za Bandari Kavu (The Tanzania Shipping Agencies Dry Port (Amendment) Regulation, 2023) Kanuni za Mawakala wa Forodha (The Tanzania Shipping Agencies Clearing & Forwarding Agents (Amendment ) Regulation, 2023 na Kanuni za Utoaji wa Huduma Ndogondogo Bandarini (The Tanzania Shipping Agencies) Miscellaneous Port Services (Amendment ) Regulations, 2023. 

Wadau waliohudhuria mkutano huu wametoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Tanzania Bara) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Visiwani) pamoja na taasisi mbalimbali nchini. 

Mgeni Rasmi katika Mkutano huo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Bi. Khadija Rajab. Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere - JNICC Dar es salaam tarehe 5 Mei, 2023.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo