Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC YAKUTANA NA WADAU KUPITIA TAARIFA YA MSHAURI ELEKEZI KUHUSU MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA WADAU WA BANDARI YA DAR ES SALAAM NA SHOROBA ZA USAFIRISHAJI

Imewekwa: 06 October, 2025
TASAC YAKUTANA NA WADAU KUPITIA TAARIFA YA MSHAURI ELEKEZI KUHUSU MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA WADAU WA BANDARI YA DAR ES SALAAM NA SHOROBA ZA USAFIRISHAJI

Shirika la Uwakala Wa Meli Tanzania (TASAC) tarehe 02, 2025 limekutana na wadau wa bandari kupokea taarifa ya mshauri elekezi kuhusu Makubaliano ya Ushurikiano wa Wadau wa Bandari ya Dar es Salaam na Shoroba za Usafirishaji "Dar es Salaam Port and Transport Corridors Community Charter" katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF uliopo Mtaa wa Garden, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Nahson Sigalla ameeleza kuwa lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kupata maoni ili kuboresha taarifa hiyo ili wadau wote  wawe na lengo la kupata chata iliyo bora.

“Kuna umuhimu wa taasisi zote kuwianishwa kwa pamoja na wadau wengine ili kupata matokeo bora hili hii chata ilete ufanisi katika bandari na shoroba ambazo zinaunga bandari yetu na maeneo mengine ambapo shehena inakwenda au inatoka,” amesema Bw. Sigalla.

Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya kuandaa makubaliano ya Jumuiya ya Bandari ya Dar es Salaam na sharoba zake, Bw. Clement Kamindu amewashukuru wadau wote kwa maoni waliyoyatoa na wanayoendelea kuyatoa na kutoa wito kwa wadau hao kuendelea kuboresha chata hiyo kwa kuwa ni ya wadau wote na si mtu mmoja.

Kikao hicho cha wadau kilihudhuriwa na Wenyeviti wa Bodi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nah. Mussa Mandia pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Ally Karavina ambapo kwa upande wao waliupongeza mchakato mzima na kutoa baraka zao katika utekelezaji wa kazi kwa kushirikiana baina ya wadau, huku wakisisitiza umuhimu wa kufuata sheria ya pamoja ya ushoroba huo.

Wadau wengine walioshiriki ni kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Wizara ya Kilimo, Mamlaka ya Hali ya Hewa, DP World, Chama cha Waendeshaji Bandari Kavu (CIDAT), na Vyama vya Mawakala wa Forodha (TAFFA, TACAS na CALAT) pamoja na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji majini.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo