Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

TASAC yakutana na Idara ya Ajira za Mabaharia Bahamas, Uingereza kujadili masuala mbalimbali ya sekta ya usafiri majini hususan kutambuliana vyeti

Imewekwa: 08 June, 2023
TASAC yakutana na Idara ya Ajira za Mabaharia Bahamas, Uingereza kujadili masuala mbalimbali ya sekta ya usafiri majini hususan kutambuliana vyeti

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge (Wa katikati) na Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dkt. Tumaini S. Gurumo (Wa kwanza Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ajira za Mabaharia, Capt. Oli Olsen (Wa kwanza Kulia) walipokutana katika Ofisi za Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS, mjini London, Uingereza tarehe 05 Juni, 2023 kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya sekta ya usafiri majini hususani kutambuliana vyeti vya mabaharia na mafunzo kati ya TASAC na Mamlaka hiyo. Halikadhalika, mabaharia wa kitanzania kupatiwa mafunzo katika meli zilizosajiliwa na Mamlaka hiyo.

Katika kikao kifupi kilichofanyika kati ya Mamlaka hizo, Capt. Oli kwa niaba ya Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS ameahidi kushirikiana na Mamlaka zinazosimamia masuala ya Mabaharia nchini Tanzania hususan katika maeneo ya kutambualiana vyeti na mafunzo ili kukuza sekta ya usafiri majini nchini Tanzania.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo