TASAC yaibuka kinara Uandaaji wa taarifa ya Mahesabu kwa viwango vya Kimataifa.
TASAC yaibuka kinara Uandaaji wa taarifa ya Mahesabu kwa viwango vya Kimataifa.
Imewekwa: 16 January, 2024
TASAC imepokea tuzo hiyo kwa kushika nafasi ya kwanza katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa ya mahesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa mwaka 2022 kati ya Mamlaka 9 za Udhibiti zilizoshindanishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu nchini.
Tuzo hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali tarehe 01 Disemba, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Ikumbukwe TASAC imeshika nafasi ya kwanza kwa mara ya pili, mara ya kwanza ilishika nafasi hiyo mwaka 2021.